-
Bwana wa Kweli Aja kwa Ajili ya HukumuMnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
-
-
Yehova hawaoni kwa mchezo tu wale wanaodharau mpango wa ndoa. Kinyume cha sheria ya Mungu, wanaume wa Yuda wametwaa wake wa kigeni. (Kumbukumbu 7:3, 4) Wameshughulika kwa hila na wake za ujana wao kwa kuwataliki. Yehova “amechukia kutaliki,” Malaki anaonya.—2:10-17, NW.
-
-
Bwana wa Kweli Aja kwa Ajili ya HukumuMnara wa Mlinzi—1989 | Julai 1
-
-
○ 2:13—Waume wengi Wayahudi walikuwa wakitaliki wake za ujana wao, labda ili wafunge ndoa na wanawake vijana zaidi wa kipagani. Madhabahu ya Yehova ikafunikwa na machozi—kwa uwazi hayo yakiwa ni yale ya wake waliokataliwa ambao walikuja patakatifu kumimina kihoro chao mbele za Mungu.—Malaki 2:11, 14, 16.
-