-
Yehova—Chanzo cha Haki na Uadilifu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
11. (a) Kwa nini Mafarisayo walimwuliza Yesu kuhusu kuponya siku ya Sabato? (b) Jibu la Yesu lilifunua nini?
11 Wakati wa huduma yake ya Galilaya katika masika ya mwaka wa 31 W.K., Yesu alimwona mtu mwenye mkono ulionyauka katika sinagogi. Kwa kuwa ilikuwa siku ya Sabato, Mafarisayo wakamwuliza Yesu: “Je, yaruhusika kisheria kuponya siku ya Sabato?” Badala ya kuhangaishwa kikweli na kuteseka kwa yule mtu maskini, walikuwa na tamaa ya kutafuta kisingizio cha kumlaumu Yesu, kama vile swali lao lilivyoonyesha. Si ajabu Yesu aliombolezea hali yao ya mioyo isiyo na hisia! Kisha akauliza Mafarisayo hao swali kama hilohilo: “Je, yaruhusika kisheria siku ya sabato kutenda kitendo chema?” Waliponyamaza, Yesu alijibu swali lake mwenyewe kwa kuuliza kama hawangemwokoa kondoo aliyeanguka shimoni siku ya sabato.b “Binadamu ni mwenye thamani zaidi sana kama nini kuliko kondoo!” Yesu alisababu, kwa mantiki isiyokanushika. “Kwa hiyo yaruhusika kisheria kufanya jambo bora siku ya sabato,” akamalizia. Haki ya Mungu haipaswi kuzuiwa kamwe na mapokeo ya binadamu. Akiwa ameelewesha jambo hilo, Yesu aliuponya mkono wa yule mwanamume.—Mathayo 12:9-13; Marko 3:1-5.
-
-
Yehova—Chanzo cha Haki na Uadilifu wa KweliMnara wa Mlinzi—1998 | Agosti 1
-
-
b Yesu alichagua kielelezo bora kwa sababu sheria ya mdomo ya Wayahudi iliwaruhusu hasa kusaidia mnyama aliyekuwa katika taabu siku ya sabato. Katika pindi nyingine kadhaa, kulikuwa na mabishano kuhusu suala hilohilo, yaani, kama iliruhusiwa kisheria kuponya siku ya Sabato.—Luka 13:10-17; 14:1-6; Yohana 9:13-16.
-