Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mtazamo-Kimbele wa Utukufu wa Ufalme wa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Januari 1
    • YESU amesimama akiwa njiani kwenda Kaisaria Filipi, na yeye anafundisha kutano la watu pamoja na mitume wake. Yeye anafanya tangazo hili la kuwagutusha: “Kwa kweli mimi nasema kwenu ninyi kwamba pana baadhi ya wale ambao wanasimama hapa ambao hawataonja kifo hata kidogo mpaka kwanza wao waone yule Mwana wa binadamu akija katika Ufalme wake.”

      Yesu angeweza kuwa anamaanisha nini? lazima wanafunzi wawe wanashangaa wakitaka kujua. Karibu juma moja baadaye, Yesu anachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye na wao wanapanda mlima mrefu sana. Inawezekana kuwa ni usiku, kwa kuwa wale wanafunzi ni wenye usingizi. Wakati Yesu anaposali, yeye anageuka sura mbele yao. Uso wake unaanza kung’aa kama jua, na mavazi yake yanakuwa maangavu kama nuru.

  • Mtazamo-Kimbele wa Utukufu wa Ufalme wa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—1988 | Januari 1
    • Njozi hiyo inathibitika kuwa yenye kutia nguvu kama nini, kwa wote Yesu na wanafunzi wale! Ile njozi ni, kama inavyoweza kusemwa, utangulizi wa maono ya utukufu wa ufalme wa Kristo. Wale wanafunzi ni kama kwa kweli waliona yule “Mwana wa mtu akija katika ufalme wake,” sawasawa na vile Yesu alikuwa ameahidi juma moja mapema. Baada ya kifo cha Yesu, Petro aliandika juu ya wao kuwa walikwisha ‘kuwa mashahidi wenye kujionea kwa macho utukufu wa adhama ya Kristo wakati sisi tulipokuwa pamoja na yeye katika ule mlima mtakatifu.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki