Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mkiwiwa Kodi, Lipeni Kodi”
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Novemba 15
    • Kuwa mtu asiyelaumika. Waangalizi wa Kikristo ni lazima wawe ‘wasiolaumika’ ili wastahili cheo chao. Vivyo hivyo, kutaniko lote lapaswa liwe lisilolaumika machoni pa Mungu. (1 Timotheo 3:2; linganisha Waefeso 5:27.) Kwa hiyo wao hujaribu kudumisha sifa nzuri katika jumuiya, hata kama ni habari ya kulipa kodi. Yesu Kristo mwenyewe aliweka kielelezo kizuri katika habari hii. Mwanafunzi wake Petro aliulizwa kama Yesu alilipa kodi ya hekalu, jambo dogo la drakma mbili tu. Kwa kweli, Yesu hakupaswa kulipa kodi hiyo, kwa kuwa hekalu lilikuwa nyumba ya Baba yake na hakuna mfalme atozaye mwana wake kodi. Yesu alisema hivyo; lakini alilipa kodi hiyo. Kwa kweli, yeye hata alitumia mwujiza kutoa pesa iliyohitajika! Kwa nini alipe kodi ambayo yeye kwa kufaa hakupaswa kulipa? Kama Yesu mwenyewe alivyosema, ilikuwa kwamba “tusije tukawakwaza.”—Mathayo 17:24-27.b

  • “Mkiwiwa Kodi, Lipeni Kodi”
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Novemba 15
    • b Kwa kupendeza, ni Gospeli ya Mathayo pekee iliyorekodi tukio hili katika maisha ya duniani ya Yesu. Kwa kuwa mbeleni Mathayo mwenyewe alikuwa mtoza kodi, bila shaka alivutiwa sana na mtazamo wa Yesu juu ya jambo hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki