Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
    • “Na ndugu yako akikukosea, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa [“kutaniko,” NW]; na asiposikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.”—Mathayo 18:15-17.

  • Wewe Husuluhishaje Matatizo?
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Julai 15
    • Ikiwa jambo hilo halingeweza kusuluhishwa, lingepelekwa kutanikoni. Zamani, jambo hilo lilimaanisha wazee wa Wayahudi lakini baadaye, ikawa wazee wa kutaniko la Kikristo. Huenda mtenda-kosa alilazimika kufukuzwa kutanikoni. Hilo ndilo linalomaanishwa na “kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru,” watu ambao Wayahudi waliepuka. Hatua hiyo nzito haingechukuliwa na Mkristo yeyote mmoja-mmoja. Wazee waliowekwa rasmi, wanaowakilisha kutaniko, pekee ndio wana mamlaka ya kuchukua hatua kama hiyo.—Linganisha 1 Wakorintho 5:13.

      Uwezekano wa mtenda-kosa asiyetubu kutengwa na ushirika waonyesha kwamba Mathayo 18:15-17 halisemi juu ya matatizo madogo-madogo. Yesu alikuwa akirejezea makosa mazito, na ambayo yangesuluhishwa kati ya watu wawili wanaohusika. Kwa kielelezo, kosa laweza kuwa uchongezi, likiharibu kabisa sifa ya mchongewa. Au laweza kuhusika na mambo ya kifedha, kwa sababu mistari ifuatayo ina kielezi cha Yesu juu ya mtumwa mkatili aliyekuwa amesamehewa deni kubwa. (Mathayo 18:23-35) Mkopo usiolipwa kwa wakati uliotakikana waweza kuwa tu tatizo la muda liwezalo kusuluhishwa kati ya watu wawili. Lakini laweza kuwa dhambi nzito, yaani, wizi, ikiwa mwenye deni akataa kwa ukaidi kulipa deni lake.

      Dhambi nyingine haziwezi kusuluhishwa kati ya Wakristo wawili tu. Kulingana na Sheria ya Musa, dhambi nzito zilikuwa ziripotiwe. (Mambo ya Walawi 5:1; Mithali 29:24) Vivyo hivyo, dhambi nzito ihusuyo utakaso wa kutaniko ni lazima iripotiwe kwa wazee wa Kikristo.

      Lakini, visa vingi vya kutoelewana kati ya Wakristo havihusiki na hatua hiyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki