Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuangaza Nuru Juu ya Kuwapo kwa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Mei 1
    • 8, 9. (a) Kuwapo kwa Yesu kifalme kunatia ndani nini? (b) Unabii wa Yesu kuhusu Makristo wawongo unaonyesha nini kuhusu mahali na jinsi ya kuwapo kwake?

      8 Kwa kuwa umaliki wa Yesu unatia ndani dunia yote, ibada ya kweli inapanuliwa kwenye mabara yote. Kuwapo (pa·rou·siʹa) kwake kifalme ni wakati wa ukaguzi wa tufeni pote. (1 Petro 2:12) Lakini, je, kuna jiji kuu au kitovu ambako Yesu aweza kuendewa? Yesu alijibu hilo kwa kutabiri kwamba wakati wa kutazamia kuwapo kwake, Makristo wawongo wangetokea. Yeye alionya: “Basi wakiwaambia, [Kristo] Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja [kuwapo, NW, pa·rou·siʹa] kwake Mwana wa Adamu.”—Mathayo 24:24, 26, 27.

  • Kuangaza Nuru Juu ya Kuwapo kwa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—1993 | Mei 1
    • 10. Meme za kweli ya Biblia zimemwekaje tufeni pote?

      10 Kinyume cha hivyo, hakungekuwa na chochote cha kuficha kuhusu kuja kwa Yesu akiwa Mfalme, mwanzoni mwa kuwapo kwake kifalme. Kama vile Yesu alivyotabiri, meme za kweli ya Biblia zinaendelea kumweka (kumulika) kwenye maeneo mapana kutoka sehemu za mashariki hadi sehemu za magharibi, tufeni pote. Kweli kweli, wakiwa wachukuaji nuru wa ki-siku-hizi, Mashahidi wa Yehova wanathibitika kuwa ‘nuru ya mataifa, ili wapate kuwa wokovu [wa Yehova] hata miisho ya dunia.’—Isaya 49:6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki