Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Utasimamaje Mbele ya Kiti cha Hukumu?
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Oktoba 15
    • 21 Lakini, itakuwaje kwa watu katika mataifa hayo Mwana wa binadamu afikapo katika utukufu wake? Ebu tuone kutokana na mfano wa kondoo na mbuzi, unaoanza kwa maneno haya: “Wakati Mwana wa binadamu awasilipo katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapoketi juu ya kiti chake cha ufalme chenye utukufu. Na mataifa yote yatakusanywa mbele yake.”—Mathayo 25:31, 32, NW.

      22, 23. Ni mambo yapi yaonyeshayo kwamba mfano wa kondoo na mbuzi haukuanza kutimizwa katika 1914?

      22 Je, mfano huu unahusu wakati Yesu alipoketi katika mamlaka ya kifalme katika 1914, kama ambavyo tumeelewa kwa muda mrefu? Naam, Mathayo 25:34 lasema juu yake akiwa Mfalme, kwa hiyo kwa kupatana na akili mfano huu wahusu tangu wakati Yesu alipokuwa Mfalme katika 1914. Lakini ni hukumu gani aliyofanya upesi baadaye? Haikuwa hukumu ya “mataifa yote.” Badala ya hivyo, alielekeza uangalifu wake kwa wale wanaodai kufanyiza “nyumba ya Mungu.” (1 Petro 4:17, italiki ni zetu.) Kwa kupatana na Malaki 3:1-3, Yesu, akiwa mjumbe wa Yehova, alikagua kihukumu Wakristo watiwa-mafuta waliosalia duniani. Pia ulikuwa wakati wa kutoa adhabu ya kihukumu juu ya Jumuiya ya Wakristo, waliodai kwa uwongo kuwa “nyumba ya Mungu.”c (Ufunuo 17:1, 2; 18:4-8) Lakini hakuna chochote kionyeshacho kwamba wakati huo, au tangu wakati huo, Yesu aliketi ili kuhukumu watu wa mataifa yote hatimaye kuwa kondoo au mbuzi.

      23 Tukichanganua utendaji wa Yesu katika mfano huu, twamwona hatimaye akihukumu mataifa yote. Mfano huu hauonyeshi kwamba kuhukumu huko kungeendelea kwa kipindi kirefu cha miaka mingi, kana kwamba kila mtu aliyekufa katika miongo hii ambayo imepita alihukumiwa kustahili kifo kidumucho milele au uhai udumuo milele. Yaonekana kwamba wengi ambao wamekufa katika miongo ya majuzi wameenda katika kaburi la kawaida la wanadamu. (Ufunuo 6:8; 20:13) Hata hivyo, huu mfano waonyesha wakati ambapo Yesu ahukumu watu wa “mataifa yote” ambao wakati huo wako hai na wanakabili utekelezaji wa adhabu yake ya kihukumu.

  • Kuna Wakati Ujao Gani kwa Kondoo na Mbuzi?
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Oktoba 15
    • “Atatenganisha watu, kama vile mchungaji atenganishavyo kondoo na mbuzi.”—MATHAYO 25:32, NW.

  • Kuna Wakati Ujao Gani kwa Kondoo na Mbuzi?
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Oktoba 15
    • 3. Mapema katika maneno yake, Yesu alisema nini kingetukia mara tu baada ya dhiki kubwa kuanza?

      3 Yesu alitabiri matukio makubwa ambayo yangetukia “mara baada ya” kufyatuka kwa dhiki kubwa, matukio tunayongoja. Alisema kwamba ndipo “ishara ya Mwana wa binadamu” itatokea. Hili litaathiri kabisa “makabila yote ya dunia” ambayo “yatamwona Mwana wa binadamu akija juu ya mawingu ya mbinguni na nguvu na utukufu mkubwa.” Mwana wa binadamu ataandamana na “malaika zake.” (Mathayo 24:21, 29-31, NW)a Vipi juu ya mfano wa kondoo na mbuzi? Biblia za kisasa huuweka katika sura ya 25, lakini huo ni sehemu ya jibu la Yesu, ukieleza mambo mengine zaidi kuhusu kuja kwake katika utukufu na kukazia hukumu yake juu ya “mataifa yote.”—Mathayo 25:32, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki