-
“Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
-
-
15-17. (a) Baba huyo alitendaje alipomwona mwana wake? (b) Kanzu, pete, na makubazi ambayo baba alimvika mwana wake vinamaanisha nini? (c) Baba anaonyesha nini kwa kutayarisha karamu?
15 “Alipokuwa angali mbali sana, baba yake alimwona mara hiyo naye akasukumwa na sikitiko, naye akakimbia akaangukia shingo yake na kumbusu kwa wororo. Ndipo yule mwana akamwambia, ‘Baba, nimefanya dhambi dhidi ya mbingu na dhidi yako. Sistahili tena kuitwa mwana wako. Unifanye niwe kama mmoja wa wanaume wako walioajiriwa.’ Lakini yule baba akawaambia watumwa wake, ‘Upesi! leteni nje kanzu, iliyo bora zaidi, mmvike hiyo, na mtie pete mkononi mwake na makubazi miguuni mwake. Nanyi leteni fahali mchanga aliyenoneshwa, mchinjeni na acheni tule na kujifurahisha wenyewe, kwa sababu huyu mwana wangu alikuwa amekufa naye akaja tena kwenye uhai; alikuwa amepotea naye akapatikana.’ Nao wakaanza kujifurahisha wenyewe.”—Luka 15:20-24.
-
-
“Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
-
-
17 Baba alipomfikia mwana wake, alimwangukia shingoni na kumbusu kwa wororo. Kisha akaamuru watumwa wake wamvike kanzu, pete, na makubazi. Kanzu hiyo haikuwa vazi la kawaida tu, bali ilikuwa kanzu “iliyo bora zaidi,” labda aina ya vazi rasmi lililorembeshwa sana ambalo lilitolewa kwa mgeni mheshimiwa. Kwa kuwa kwa kawaida pete na makubazi hayakuvaliwa na watumwa, baba alikuwa akidhihirisha kwamba mwana wake alikuwa akikaribishwa arudi akiwa mshiriki kamili wa familia. Lakini baba alifanya mengi hata zaidi. Aliagiza kuwe na karamu ya kusherehekea kurudi kwa mwana wake. Kwa wazi, mwanamume huyu hakumsamehe mwana wake shingo upande au kwa sababu kurudi kwake kulimlazimisha afanye hivyo; alitaka kumsamehe. Jambo hilo lilimfanya ashangilie.
-