-
Kuifikia Mioyo ya Watu wa Ukoo Wasio WaaminiMnara wa Mlinzi—2014 | Machi 15
-
-
Katika karne ya kwanza, Andrea alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutambua kwamba Yesu ndiye Masihi. Alimwambia nani habari hiyo mara moja? “Kwanza huyu [Andrea] alimpata ndugu yake mwenyewe, Simoni, na kumwambia: ‘Tumempata Masihi’ (ambalo linapotafsiriwa humaanisha, ‘Kristo’).” Andrea alimpeleka Petro kwa Yesu, na hivyo Petro akapata nafasi ya kuwa mwanafunzi wa Yesu.—Yoh. 1:35-42.
-
-
Kuifikia Mioyo ya Watu wa Ukoo Wasio WaaminiMnara wa Mlinzi—2014 | Machi 15
-
-
Tunajifunza nini kutokana na jinsi Andrea na Kornelio walivyowatendea watu wao wa ukoo?
Andrea na Kornelio walichukua hatua ya kuwasaidia. Andrea alimtambulisha Petro kibinafsi kwa Yesu, naye Kornelio alifanya mipango ili watu wake wa ukoo wamsikilize Petro. Hata hivyo, Andrea na Kornelio hawakutumia ujanja au kuwashinikiza watu wao wa ukoo kuwa wafuasi wa Kristo. Tunajifunza nini? Itakuwa vyema tukiwaiga. Tunaweza kuongea na watu wetu wa ukoo mambo fulani tuliyojifunza na hivyo kuwapa nafasi ya kujifunza kweli za Biblia na kuwafahamu waamini wenzetu. Hata hivyo, tunapaswa kuheshimu uhuru wao wa kuchagua na kutowashinikiza kujifunza. Ili tuone jinsi tunavyoweza kuwasaidia watu wetu wa ukoo, fikiria mfano wa Jürgen na Petra, wenzi wa ndoa wanaoishi Ujerumani.
-