Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Wakajazwa Roho Takatifu”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • “Wayahudi na pia wageuzwa imani” walimsikiliza Petro akihubiri katika siku ya Pentekoste ya mwaka 33 W.K.​—Matendo 2:10.

      Nikolao ambaye alikuwa mmoja wa wanaume waliowekwa rasmi juu ya ‘kazi muhimu’ ya kugawa chakula kila siku, anatajwa kuwa “mgeuzwa-imani wa Antiokia.” (Matendo 6:3-5) Wageuzwa imani walikuwa watu wa mataifa mengine, wasio Wayahudi, ambao walijiunga na dini ya Kiyahudi. Walionwa kuwa Wayahudi, kwa sababu walimkubali Mungu wa Israeli na kuikubali Sheria ya Waisraeli, walikataa miungu mingine yote, (wanaume) walitahiriwa, nao walijiunga na taifa la Israeli.

      Baada ya Wayahudi kutoka uhamishoni Babiloni mwaka wa 537 K.W.K., wengi wao waliishi mbali na nchi ya Israeli lakini waliendelea kuwa wafuasi wa dini ya Kiyahudi. Hivyo, watu wengi katika maeneo ya Mashariki ya Kati na hata mbali zaidi wakaifahamu dini ya Kiyahudi. Waandikaji wa zamani, kama vile, Horace na Seneca, wanaeleza kwamba watu wengi wa nchi mbalimbali waliovutiwa na Wayahudi na imani zao, walijiunga nao na kuwa wageuzwa imani.

  • “Wakajazwa Roho Takatifu”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
    • Kuna hati zinazothibitisha kwamba Wayahudi waliishi Misri angalau kuanzia karne ya sita K.W.K. Wakati huo Yeremia alituma ujumbe kwa Wayahudi walioishi katika sehemu mbalimbali za Misri, kutia ndani Memfisi. (Yer. 44:1, maelezo ya chini) Kuna uwezekano kwamba watu wengi walihamia Misri wakati wa utawala wa Ugiriki. Mwanahistoria Yosefu anasema kwamba Wayahudi walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuishi Aleksandria. Baada ya muda, walimiliki sehemu kubwa ya jiji hilo. Katika karne ya kwanza W.K., Philo mwandishi Myahudi, alidai kwamba Wayahudi milioni moja hivi walikuwa wakiishi katika maeneo mbalimbali nchini Misri, “kuanzia Libya hadi Ethiopia.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki