Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Piga Mbiu ya Ufalme wa Yehova kwa Ujasiri!
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Juni 15
    • 7. Paulo aliwekaje kielelezo katika kujitiisha kwa mapenzi ya Mungu?

      7 Safari ya tatu ya Paulo ya kimisionari ilipokuwa ikikaribia kumalizika (karibu 56 W.K.), yeye aliweka kielelezo kizuri katika kujitiisha kwa mapenzi ya Mungu. (21:1-14, NW) Katika Kaisaria yeye na waandamani wake walikaa pamoja na Filipo, ambaye binti zake wanne walio mabikira ‘walitoa unabii,’ wakitabiri matukio kwa roho takatifu. Huko nabii Mkristo Agabo akafunga mikono na nyayo zake mwenyewe kwa ukanda wa Paulo na kusukumwa na roho kusema kwamba Wayahudi wangemfunga mwenye ukanda huo katika Yerusalemu na kumtia mikononi mwa Wasio Wayahudi. “Niko tayari si kufungwa tu bali pia kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu,” akasema Paulo. Wanafunzi wakaafikiana naye, wakisema: “Acha mapenzi ya Yehova yatendeke.”

  • Piga Mbiu ya Ufalme wa Yehova kwa Ujasiri!
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Juni 15
    • 9. Kwa habari ya jeuri ya wafanya ghasia, kuna ulinganifu gani kati ya maono ya Paulo na yale ya Mashahidi wa Yehova leo?

      9 Mara nyingi Mashahidi wa Yehova wameshika ukamilifu kwa Mungu kwa kukabiliana na jeuri ya wafanya ghasia. (Kwa kielelezo, ona Kitabu cha Mwaka 1982-85 cha Mashahidi wa Yehova, kurasa 110-6.) Vivyo hivyo Wayahudi kutoka Esia Ndogo walichochea kitendo cha wafanya ghasia dhidi ya Paulo. (21:27-40) Kwa kumwona Trofimo Mwefeso akiwa pamoja naye, walimshtaki mtume kwa ubandia juu ya kunajisi hekalu kwa kuingiza Wagiriki humo. Paulo alikuwa karibu kuuawa wakati ofisa-mtetezi Mroma Klaudio Lisia na watu wake walipokandamiza fujo hiyo! Kama ilivyotabiriwa (lakini ikasababishwa na Wayahudi), Lisia aliagiza Paulo afungwe minyororo. (Matendo 21:11) Mtume alikuwa karibu kupelekwa ndani ya makao ya askari yenye kuungana na ua wa hekalu wakati Lisia alipopata habari kwamba Paulo si mfitini serikali bali ni Myahudi aliyeruhusiwa kuingia eneo la hekalu. Alipopata ruhusa ya kusema, Paulo alihutubia watu hao kwa Kiebrania.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki