-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
Wale ‘wanaume wenye kutumia visu’ waliokuwapo Paulo alipokamatwa na Waroma walikuwa nani?
▪ Kitabu cha Matendo kinasema kwamba fujo zilipotokea katika hekalu huko Yerusalemu, kiongozi wa kikosi cha askari-jeshi Waroma alimkamata mtume Paulo huku akiamini kwamba alikuwa kiongozi wa kikundi cha uasi cha “wanaume elfu nne wenye kutumia visu.” (Matendo 21:30-38) Tunajua nini kuhusu wanaume hao wenye kutumia visu?
Neno la Kigiriki ambalo limetafsiriwa kuwa ‘wanaume wenye kutumia visu’ linatokana na neno sicarii la Kilatini ambalo linamaanisha “watu wanaotumia sica,” au kisu. Mwanahistoria wa karne ya kwanza Flavio Yosefo anasema kwamba Sicarii kilikuwa kikundi cha Wayahudi sugu wazalendo, maadui wakali sana wa Roma, ambao walipanga mauaji ya kisiasa.
Yosefo anasema kwamba Sicarii “waliwachinja watu mchana, katikati ya mji; walifanya hivyo hasa kwenye sherehe, walipochangamana na umati wa watu. Na walificha katika nguo zao visu ambavyo walitumia kuwadunga maadui wao.” Adui alipoanguka chini na kufa, Sicarii walijifanya kwamba wamekasirishwa na mauaji hayo ili wasigunduliwe. Yosefo anaongezea kwamba baadaye Sicarii waliwachochea Wayahudi kuasi serikali ya Roma katika mwaka wa 66-70 W.K. Ndiyo sababu yule kiongozi wa kikosi cha Roma alitaka sana kumkamata yule aliyedaiwa kuwa kiongozi wa kikundi hicho.
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2010 | Machi 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 15]
Mchoro wa mwanamume mwenye kutumia kisu
-