-
Majuma SabiniUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Makosa na dhambi zakomeshwa. Kukatiliwa mbali kwa Yesu katika kifo, ufufuo wake, na kuonekana kwake mbinguni kulitokeza ‘ukomeshaji wa makosa, na kumaliza kabisa dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya kosa.’ (Da 9:24) Agano la Sheria lilikuwa limewafunua Wayahudi kuwa watenda-dhambi, likawahukumu kuwa hivyo, na kuleta juu yao laana ya kuwa wavunja-agano. Lakini mahali ambapo dhambi ‘ilizidi’ ikiwa imefunuliwa au kudhihirishwa na Sheria ya Musa, rehema na kibali cha Mungu vilizidi zaidi kupitia Masihi. (Ro 5:20) Kupitia dhabihu ya Masihi, makosa na dhambi ya watenda-dhambi wenye kutubu yanaweza kufutiliwa mbali na adhabu yake kuondolewa.
-
-
DhambiUfahamu wa Kina wa Maandiko
-
-
Kwa hiyo, wakati wa kipindi cha mababu wa ukoo kuanzia Abrahamu hadi wale wana 12 wa Yakobo, Maandiko yanaonyesha wanadamu wa rangi na mataifa mengi wakisema juu ya “dhambi” (chat·taʼth′), kama vile dhambi dhidi ya mwajiri (Mwa 31:36), dhidi ya mtawala anayemtawala mtu (Mwa 40:1; 41:9), dhidi ya mtu wa ukoo (Mwa 42:22; 43:9; 50:17), au dhidi ya binadamu mwenziwe tu (Mwa 20:9). Vyovyote vile, mwenye kutumia neno hilo alikiri pale alipolitumia kuwa na uhusiano fulani pamoja na mtu ambaye dhambi hiyo ilifanywa au huenda ikatendwa dhidi yake na alitambua daraka lenye kuambatana la kuheshimu masilahi ya mtu huyo au mapenzi na mamlaka yake, kama vile katika kisa cha mtawala, na kutotenda kinyume chake. Kwa njia hiyo walionyesha kuna uthibitisho wa asili ya adili. Hata hivyo, wakati ulipopita, utawala wa dhambi juu ya wale wasiomtumikia Mungu uliimarika, hivi kwamba Paulo akaweza kusema juu ya watu wa mataifa ni kana kwamba wanatembea katika ‘katika giza kiakili, na kutenganishwa mbali na uzima ambao ni wa Mungu wakiwa wameishiwa na ufahamu wote wa maadili.’—Efe 4:17-19.
-