-
Kwa Nini Mungu Ameruhusu Uovu?Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
-
-
8. Paulo anatuhimiza tufikirie mambo yapi?
8 Katika barua yake kwa Waroma, mtume Paulo auliza swali hili: “Je, kwa Mungu kuna ukosefu wa haki?” Kisha anajibu hivi kwa mkazo: “Hilo lisipate kuwa hivyo kamwe!” Kisha anakazia rehema ya Mungu na kutaja tena sababu ya Yehova kumruhusu Farao aishi kwa muda. Paulo pia aonyesha kwamba sisi wanadamu ni kama udongo mikononi mwa mfinyanzi. Halafu anasema: “Basi, ikiwa Mungu, ingawa anayo nia ya kuonyesha hasira ya kisasi yake na kujulisha nguvu yake, alivumilia kwa ustahimilivu mwingi vyombo vya hasira ya kisasi vilivyofanywa kufaa kwa ajili ya uharibifu, ili apate kujulisha utajiri wa utukufu wake juu ya vyombo vya rehema, alivyotayarisha kimbele kwa ajili ya utukufu, yaani, sisi, alioita si kutoka miongoni mwa Wayahudi tu bali pia kutoka miongoni mwa mataifa, kuna ubaya gani?”—Waroma 9:14-24.
-
-
Kwa Nini Mungu Ameruhusu Uovu?Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
-
-
10. Kwa nini Yehova amewastahimili waovu kwa miaka 1,900 iliyopita?
10 Tangu Yesu alipofufuliwa zaidi ya miaka 1,900 iliyopita, Yehova amekuwa akistahimili “vyombo vya hasira,” akiahirisha uharibifu wao. Kwa nini? Kwanza, ni kwa sababu amekuwa akiwatayarisha wale ambao watatawala pamoja na Yesu Kristo katika Ufalme wake wa mbinguni. Watu hao 144,000, ni “vyombo vya rehema” ambavyo vinatajwa na mtume Paulo. Wayahudi ndio walioalikwa kwanza wawe washiriki wa jamii hiyo ya kimbingu. Baadaye, Mungu aliwaalika watu wasio Wayahudi. Yehova hajamlazimisha yeyote kati yao amtumikie. Lakini aliwapa baadhi ya wale waliothamini mipango yake nafasi ya pekee ya kutawala pamoja na Mwanaye katika Ufalme wa mbinguni. Sasa matayarisho ya jamii hiyo ya kimbingu yanakaribia kumalizika.—Luka 22:29; Ufunuo 14:1-4.
-