Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Unangojea “Jiji Lililo na Misingi ya Kweli”?
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Agosti
    • Abrahamu akimsaidia Sara kushuka kwenye ngamia. Nyuma yao, watumishi wachache wanaendelea na shughuli zao za kila siku.

      Abrahamu alionyeshaje imani katika ahadi za Yehova? (Tazama fungu la 5)

      5. Tunajuaje kwamba Abrahamu alikuwa akingojea “jiji” ambalo mbuni wake ni Mungu?

      5 Abrahamu alionyeshaje kwamba alikuwa akingojea Ufalme, au “jiji,” ambalo mbuni wake ni Mungu? Kwanza, Abrahamu hakuwa raia wa ufalme wowote hapa duniani. Alikuwa akihama-hama kutoka eneo moja kwenda lingine, hakuwa na eneo la kudumu la kuishi na hakumuunga mkono mfalme yeyote wa kibinadamu. Kwa kuongezea, Abrahamu hakuamua kuanzisha ufalme wake mwenyewe. Badala yake aliendelea kumtii Yehova, akimngojea atimize ahadi Yake. Kwa kufanya hivyo, Abrahamu alionyesha imani ya pekee katika Yehova. Acheni tuchunguze baadhi ya changamoto alizokabili na tuone mambo tunayoweza kujifunza kutokana na mfano wake mzuri.

  • Je, Unangojea “Jiji Lililo na Misingi ya Kweli”?
    Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2020 | Agosti
    • 7. Kwa nini Abrahamu alihitaji kuwa na hakika kwamba Yehova angemlinda yeye na familia yake?

      7 Abrahamu alikuwa na uhakika kwamba Yehova angemlinda yeye na familia yake. Kwa nini? Kumbuka kwamba Abrahamu na Sara walipoondoka jiji la Uru waliacha nyumba yenye usalama na yenye kustarehesha ili wakaishi kwenye mahema kwenye eneo la wazi katika nchi ya Kanaani. Abrahamu pamoja na familia yake hawakuwa wakilindwa tena na ukuta mkubwa na handaki la maji lenye kina kirefu. Sasa hawakuwa na ulinzi dhidi ya mashambulizi ya maadui.

      8. Pindi moja Abrahamu alilazimika kukabiliana na nini?

      8 Abrahamu alifanya mapenzi ya Mungu, lakini pindi moja hakuwa na chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yake. Abrahamu alihitaji kukabiliana na njaa kali iliyopiga nchi ileile ambayo Yehova alikuwa amemtuma. Njaa hiyo ilikuwa mbaya sana hivi kwamba Abrahamu aliamua kuhamisha familia yake kwa muda kwenda Misri. Hata hivyo alipokuwa Misri, Farao, mtawala wa nchi hiyo alimchukua mke wake. Wazia wasiwasi ambao lazima Abrahamu alikuwa nao hadi Farao alipomrudisha Sara kwa Abrahamu kwa mwongozo wa Yehova.—Mwa. 12:10-19.

      9. Abrahamu alihitaji kukabiliana na changamoto gani za kifamilia?

      9 Maisha ya familia ya Abrahamu yalikuwa magumu. Sara, mke wake mpendwa, hakuweza kupata watoto. Kwa miaka mingi walihitaji kukabiliana na hali hiyo yenye kuumiza. Mwishowe, Sara akamchukua Hagari, mtumishi wake, na kumpa Abrahamu ili awazalie Abrahamu na Sara watoto. Lakini Hagari alipopata mimba ya Ishmaeli, alianza kumdharau Sara. Hali ilikuwa mbaya sana hivi kwamba Sara alimfukuza Hagari.—Mwa. 16:1-6.

      10. Ni mambo gani yaliyomhusisha Ishmaeli na Isaka yaliyojaribu imani ya Abrahamu kumwelekea Yehova?

      10 Hatimaye Sara alipata mimba na kumzalia Abrahamu mwana ambaye alimwita Isaka. Abrahamu aliwapenda wana wake wote wawili, Ishmaeli na Isaka. Lakini kwa sababu Ishmaeli alimtendea kwa njia mbaya Isaka, Abrahamu alilazimika kuwafukuza Ishmaeli na Hagari. (Mwa. 21:9-14) Baadaye, Yehova alimwomba Abrahamu amtoe Isaka kuwa dhabihu. (Mwa. 22:1, 2; Ebr. 11:17-19) Katika pindi hizo zote, Abrahamu alihitaji kuwa na uhakika kwamba mwishowe Yehova angetimiza ahadi yake kuhusu wana wake.

      11. Kwa nini Abrahamu alihitaji kumngojea Yehova kwa subira?

      11 Katika kipindi hicho chote Abrahamu alihitaji kujifunza kumngojea Yehova kwa subira. Inaelekea alikuwa na umri wa zaidi ya miaka 70 alipoondoka Uru pamoja na familia yake. (Mwa. 11:31–12:4) Na kwa miaka mia moja hivi, aliishi kwenye mahema, akihama-hama katika nchi ya Kanaani. Abrahamu alikufa akiwa na umri wa miaka 175. (Mwa. 25:7) Lakini hakuona utimizo wa ahadi ya Yehova ya kuwapa wazao wake nchi aliyokuwa akiishi. Na hakuishi vya kutosha kuliona lile jiji, yaani, Ufalme wa Mungu ukisimamishwa. Hata hivyo, Abrahamu anafafanuliwa kuwa alikufa “akiwa amezeeka na kuridhika.” (Mwa. 25:8) Licha ya changamoto zote alizokabiliana nazo, Abrahamu aliendelea kuwa na imani yenye nguvu na aliridhika kumngojea Yehova. Kwa nini aliweza kuvumilia? Kwa sababu katika maisha yote ya Abrahamu, Yehova alimlinda na kumtendea kama rafiki.—Mwa. 15:1; Isa. 41:8; Yak. 2:22, 23.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki