Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sifuni Yah kwa Hukumu Zake!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 1. Yohana anasikia maneno gani “kama sauti kubwa ya umati mkubwa katika mbingu”?

      BABULONI MKUBWA hayupo tena! Kwa kweli hizi ni habari zenye shangwe. Si ajabu kwamba Yohana anasikia mipaazo yenye furaha katika mbingu! “Baada ya vitu hivi mimi nikasikia kilichokuwa kama sauti kubwa ya umati mkubwa katika mbingu. Wao walisema: ‘Halleluyah!a Wokovu na utukufu na nguvu ni za Mungu wetu, kwa sababu hukumu zake ni za kweli na za uadilifu. Kwa maana yeye ametekeleza hukumu juu ya kahaba mkubwa ambaye alifisidi dunia kwa uasherati wake, na yeye amelipiza kisasi cha damu ya watumwa wake katika mkono wake.’ Na mara hiyo kwa mara ya pili wao wakasema: ‘Halleluyah!b Na ule moshi kutoka kwake huendelea kupaa milele na milele.’”—Ufunuo 19:1-3, NW.

      2. (a) Neno “Halleluyah” humaanisha nini, na Yohana kulisikia mara mbili kufikia hapa huonyesha nini? (b) Ni nani anayepokea utukufu kwa kuharibu Babuloni Mkubwa? Fafanua.

      2 Halleluyah kweli kweli! Neno hilo humaanisha “Sifuni Yah, nyinyi watu,” “Yah” ikiwa ni namna ya kifupi cha jina la kimungu, Yehova. Tunakumbushwa hapa waadhi ya mtunga zaburi: “Kila kitu chenye kupumua—acheni kisifu Yah. Sifuni Yah, nyinyi watu!” (Zaburi 150:6, NW) Kusikia kwa Yohana korasi ya kimbingu yenye kuchachawa ikiimba “Halleluyah!” mara mbili kufikia hapa katika Ufunuo huonyesha mwendeleo wa ufunuo wa kimungu wa ukweli. Mungu wa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo ndiye Mungu yule yule wa Maandiko ya Kiebrania ya mapema zaidi, na Yehova ndilo jina lake. Mungu aliyesababisha anguko la Babuloni wa kale amehukumu na akaharibu sasa Babuloni Mkubwa. Mpeni utukufu kwa tendo hilo la uhodari! Nguvu iliyoongoza kwa werevu kuanguka kwake ilikuwa yake badala ya kuwa ya mataifa ambayo yeye alitumia kuwa vyombo vya kumwacha ukiwa. Yatupasa sisi kumsifu Yehova pekee kwa ajili ya wokovu.—Isaya 12:2; Ufunuo 4:11; 7:10, 12.

  • Sifuni Yah kwa Hukumu Zake!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 4. Ni nini kinachofananishwa na uhakika wa kwamba moshi kutoka Babuloni Mkubwa “huendelea kupaa milele na milele”?

      4 Babuloni Mkubwa amewashwa moto kama jiji lililoshindwa, na moshi wa kutoka kwake “huendelea kupaa milele na milele.” Wakati jiji halisi linapochomwa na majeshi yenye ushindi, moshi huendelea kupaa kwa muda ambao majivu ni yenye moto. Yeyote anayejaribu kulijenga tena linapoendelea kutoa moshi atachomwa tu na yale magofu yenye kutoa moshi. Kwa kuwa moshi kutoka kwake utainuka “milele na milele” katika kuonyesha hukumu yake yenye kukata maneno, hakuna yeyote atakayeweza wakati wowote kurudisha jiji hilo lenye dhambi. Dini bandia imetoweka milele na milele. Halleluyah, kweli kweli!—Linga Isaya 34:5, 9, 10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki