Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–Magedoni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 22. Yohana anatoaje muhtasari wa mwendo wa ile vita ya mwisho?

      22 Yohana anatoa muhtasari wa mwendo wa vita hiyo ya mwisho: “Na mimi nikaona hayawani-mwitu na wafalme wa dunia na majeshi yao wamekusanyika pamoja kufanya vita na mmoja aketiye juu ya farasi na majeshi yake. Na hayawani-mwitu akabambwa, na pamoja na yeye nabii bandia ambaye alifanya mbele yake ishara ambazo kwa hizo yeye aliongoza vibaya wale ambao walipokea alama ya hayawani-mwitu na wale ambao hutoa ibada kwa mfano wake. Wakiwa wangali hai, wao wawili walivurumishwa ndani ya ziwa lenye moto ambalo huwaka salfa. Lakini wanaobaki waliuliwa mbali kwa upanga mrefu wa mmoja aketiye juu ya farasi, upanga ambao ulitokeza katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba sehemu zenye mnofu zao.”—Ufunuo 19:19-21, NW.

  • Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–Magedoni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 24. (a) Ni hukumu gani inayotekelezwa juu ya hayawani-mwitu na juu ya nabii bandia, na ni katika maana gani wao “wakiwa wangali hai”? (b) Kwa nini “ziwa la moto” lazima liwe la kitamathali?

      24 Hayawani-mwitu mwenye vichwa saba na pembe kumi kutoka katika bahari, akiwakilisha tengenezo la kisiasa la Shetani, anatumbukizwa ndani ya usahaulifu kabisa, na pamoja na yeye aenda nabii bandia, serikali ya saba ya ulimwengu. (Ufunuo 13:1, 11-13; 16:13) Wakiwa wangali “hai,” au wangali wanatenda katika umoja wao wa kuwapinga watu wa Mungu duniani, wao wanatupwa ndani ya “ziwa la moto.” Je! hili ni ziwa halisi la moto? La, kama vile hayawani-mwitu na nabii bandia wasivyokuwa wanyama halisi. Badala ya hivyo, ni ufananisho wa uharibifu kamili wa mwisho kabisa, mahali ambako hakuna kurudi. Humo ndimo, baadaye, kifo na Hadesi, pamoja na Ibilisi mwenyewe, vitavurumishwa. (Ufunuo 20:10, 14, NW) Kwa hakika si tanuri la mateso ya milele kwa waovu, kwa kuwa wazo lenyewe la mahali kama hapo ni lenye kukirihika kwa Yehova.—Yeremia 19:5; 32:35; 1 Yohana 4:8, 16.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki