-
Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–MagedoniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
22. Yohana anatoaje muhtasari wa mwendo wa ile vita ya mwisho?
22 Yohana anatoa muhtasari wa mwendo wa vita hiyo ya mwisho: “Na mimi nikaona hayawani-mwitu na wafalme wa dunia na majeshi yao wamekusanyika pamoja kufanya vita na mmoja aketiye juu ya farasi na majeshi yake. Na hayawani-mwitu akabambwa, na pamoja na yeye nabii bandia ambaye alifanya mbele yake ishara ambazo kwa hizo yeye aliongoza vibaya wale ambao walipokea alama ya hayawani-mwitu na wale ambao hutoa ibada kwa mfano wake. Wakiwa wangali hai, wao wawili walivurumishwa ndani ya ziwa lenye moto ambalo huwaka salfa. Lakini wanaobaki waliuliwa mbali kwa upanga mrefu wa mmoja aketiye juu ya farasi, upanga ambao ulitokeza katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba sehemu zenye mnofu zao.”—Ufunuo 19:19-21, NW.
-
-
Mwanavita-Mfalme Asherehekea Ushindi Kwenye Har–MagedoniUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
25. (a) Ni nani wale ambao “waliuliwa mbali kwa upanga mrefu wa mmoja aketiye juu ya farasi”? (b) Je! tutazamie kwamba hao waliouliwa mbali watakuwa na ufufuo?
25 Wengine wote ambao hawakuwa sehemu ya serikali moja kwa moja lakini hata hivyo walikuwa sehemu isiyoongoleka ya ulimwengu huu mfisadi wa aina ya binadamu, wao hali kadhalika ‘wanauliwa mbali kwa upanga mrefu wa mmoja aketiye juu ya farasi.’ Yesu atawatamka kuwa wanastahili kifo. Kwa kuwa kwa habari yao ziwa la moto halikutajwa, je! tutaraji kwamba watafufuliwa? Hakuna mahali tunapoambiwa kwamba wenye kufishwa wakati huo na Hakimu wa Yehova wanapaswa kufufuliwa. Kama Yesu mwenyewe alivyotaarifu, wote wale ambao si “kondoo” wanaenda zao “katika moto wa milele uliotayarishwa kwa ajili ya Ibilisi na malaika zake,” yaani, “katika kukatiliwa mbali kwa milele.” (Mathayo 25:33, 41, 46, NW) Hii huileta kwenye upeo “siku ya hukumu na ya kuharibiwa kwa watu wasiohofu Mungu.”—2 Petro 3:7; Nahumu 1:2, 7-9; Malaki 4:1, NW.
-