-
Maswali Kutoka kwa WasomajiMnara wa Mlinzi—2015 | Mei 15
-
-
Lakini “Gogu na Magogu” anayetajwa kwenye Ufunuo 20:8 ni nani? Wakati wa jaribu la mwisho ambalo litatokea mwishoni mwa Miaka Elfu Moja, wale watakaomwasi Yehova wataonyesha mtazamo wa uuaji kama ule wa ‘Gogu wa Magogu,’ yaani yale mataifa yatakayowashambulia watu wa Mungu mwishoni mwa dhiki kuu. Makundi yote mawili yatapata matokeo yaleyale, yaani, yataangamizwa milele! (Ufu. 19:20, 21; 20:9) Hivyo basi, inafaa kwamba wale wote watakaoasi mwishoni mwa Miaka Elfu Moja wanaitwa “Gogu na Magogu.”
-