Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 9. Yohana anaelezaje vifaa vya ujenzi vya jiji?

      9 Yohana aendeleza elezo lake: “Sasa muundo wa ukuta walo ulikuwa yaspa, na jiji lilikuwa dhahabu safi kama kioo changavu. Misingi ya kuta za jiji ilikuwa imerembwa kwa kila namna ya jiwe la thamani: msingi wa kwanza ulikuwa yaspa, wa pili safirosi, ule wa tatu kalkedoni, wa nne emeraldi, wa tano sardoniksi, wa sita sardiosi, wa saba krisolito, wa nane berulosi, wa tisa topazi, wa kumi krisoprasosi, wa kumi na moja hayakintho-buluu, ule wa kumi na mbili amethistosi. Pia, malango kumi na mawili yalikuwa lulu kumi na mbili; kila lango lilikuwa limefanyizwa kwa lulu moja. Na njia pana ya jiji ilikuwa dhahabu safi, kama kioo chenye kuona ndani.”—Ufunuo 21:18-21, NW.

      10. Ni nini kinachomaanishwa na uhakika wa kwamba jiji limejengwa kwa yaspa, dhahabu, na “kila namna ya jiwe la thamani”?

      10 Mjengo wa jiji ni wenye uzuri wa kung’aa kikweli. Badala ya vifaa vya ujenzi vya kidunia, visivyodumu kama udongo-mnamo au jiwe, sisi tunasoma juu ya yaspa, dhahabu iliyosafishwa, na “kila namna ya jiwe la thamani.” Lo! jinsi hivyo vinavyotaswiri vifaa vya ujenzi vya kimbingu! Hakuna kitu kingeweza kuwa na uzuri mno zaidi ya hilo. Sanduku la agano la kale lilikuwa limefunikwa kwa dhahabu safi, na katika Biblia elementi hii mara nyingi huwakilisha vitu ambavyo ni vizuri na vyenye thamani. (Kutoka 25:11; Mithali 25:11; Isaya 60:6, 17) Lakini Yerusalemu Jipya zima, na hata njia pana yalo, vimejengwa kwa “dhahabu safi kama kioo changavu,” kutaswiri uzuri na thamani asilia inayoshinda wazo.

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 12. Ni nini kinachoashiriwa na uhakika wa kwamba (a) misingi ya jiji imerembwa kwa vito vya thamani 12? (b) malango ya jiji ni lulu?

      12 Hata misingi ya jiji ni mizuri, ikiwa imerembwa kwa vito vya thamani 12. Hii hukumbusha akilini kuhani mkuu wa Kiyahudi, ambaye katika siku za kisherehe alivalia efodi iliyotiwa njumu za mawe yenye thamani tofautitofauti 12 ambayo kidogo yafanana na haya ambayo yameelezwa hapa. (Kutoka 28:15-21) Hakika si sadifa! Badala ya hivyo, hukazia utendaji wa kikuhani wa Yerusalemu Jipya, ambalo Yesu, Kuhani Mkuu, ndiye “taa” yalo. (Ufunuo 20:6; 21:23; Waebrania 8:1) Pia, zile manufaa za huduma ya Yesu ya ukuhani-mkuu huwasilishwa kwa aina ya binadamu kupitia Yerusalemu Jipya. (Ufunuo 22:1, 2) Malango 12 ya jiji, kila moja likiwa lulu moja ya uzuri mkubwa, hukumbusha kielezi cha Yesu kilichofananisha Ufalme na lulu moja ya thamani kubwa. Wote ambao huingia kupitia malango haya watakuwa wamekwisha onyesha uthamini wa kweli kwa ajili ya thamani za kiroho.—Mathayo 13:45, 46; linga Ayubu 28:12, 17, 18.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki