Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 17. (a) Kumiminwa kwa bakuli la tano huhusianaje na giza la kiroho ambalo sikuzote limefunika ufalme wa hayawani-mwitu? (b) Watu wanatendaje kwa kuitikia kumiminwa kwa bakuli la tano la kasirani ya Mungu?

      17 Ufalme wa hayawani-mwitu huyu umekuwa katika giza la kiroho tangu ulipoanza. (Linga Mathayo 8:12; Waefeso 6:11, 12.) Bakuli la tano linaleta tangazo la peupe lenye mkazo mkubwa juu ya giza hili. Hata linalifanyia drama, kwa kuwa bakuli hili la kasirani ya Mungu humiminwa juu ya kiti cha ufalme chenyewe cha hayawani-mwitu wa ufananisho. “Na ufalme wake ukatiwa giza, na wao wakaanza kugugunya ndimi zao kwa ajili ya maumivu yao, lakini wao wakamkufuru Mungu wa mbingu kwa ajili ya maumivu yao na kwa ajili ya vidonda vyao, na wao hawakutubu kazi zao.”—Ufunuo 16:10b, 11, NW.

  • Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye Tamati
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 19. Kupatana na Ufunuo 16:10, 11, kufichuliwa peupe kwa Shetani kuwa mungu wa huu mfumo wa mambo kunasababisha nini?

      19 Akiwa mtawala wa ulimwengu, Shetani amesababisha utofurahifu mwingi na mateso. Njaa kuu, vita, jeuri, uhalifu, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, utovu wa adili, magonjwa yenye kupitishwa kingono, utovu wa haki, unafiki wa kidini—haya na zaidi ni alama za mfumo wa mambo wa Shetani. (Linga Wagalatia 5:19-21.) Hata hivyo, ufichulio wa peupe wa Shetani kuwa ndiye mungu wa huu mfumo wa mambo ulisababisha maumivu na tahayari kwa wale ambao huishi kwa viwango vyake. “Wao wakaanza kugugunya ndimi zao kwa ajili ya maumivu yao,” hasa katika Jumuiya ya Wakristo. Wengi huona uchungu moyoni kwa vile ukweli hufunua mtindo wao wa maisha. Baadhi yao huuona kuwa tisho, nao hunyanyasa wale wanaoutangaza. Wanakataa Ufalme wa Mungu na kutusi jina takatifu la Yehova. Hali yao ya kidini yenye ugonjwa na yenye madonda madonda inafunuliwa wazi, hivi kwamba wao wanakufuru Mungu wa mbingu. La, wao ‘hawatubu kazi zao.’ Kwa hiyo sisi hatuwezi kutazamia kuongolewa kwa tungamo la watu kabla ya mwisho wa huu mfumo wa mambo.—Isaya 32:6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki