-
Kutoka 29:27, 28Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
27 Utakitakasa kidari cha toleo la kutikiswa na ule mguu wa fungu takatifu ambao ulitikiswa na ambao ulichukuliwa kutoka kwa yule kondoo dume wa kumweka rasmi kuhani,+ aliyetolewa kwa ajili ya Haruni na wanawe. 28 Vitu hivyo vitakuwa vya Haruni na wanawe kulingana na sheria ya kudumu itakayotekelezwa na Waisraeli, kwa sababu vitu hivyo ni fungu takatifu, navyo vitakuwa fungu takatifu litakalotolewa na Waisraeli.+ Ni fungu lao takatifu kwa Yehova kutoka katika dhabihu zao za ushirika.+
-
-
Kumbukumbu la Torati 18:3Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
3 “Sasa hii ndiyo haki ambayo makuhani wanastahili kutoka kwa watu: Mtu yeyote anayetoa dhabihu, iwe ni ng’ombe dume au kondoo anapaswa kumpa kuhani mguu wa mbele, mataya, na tumbo.
-
-
1 Wakorintho 9:13Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
13 Je, hamjui kwamba watu wanaofanya kazi takatifu hula vitu vya hekalu, na kwamba wale wanaohudumu kwa kawaida kwenye madhabahu hupata fungu lao kutoka kwenye madhabahu?+
-