Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hesabu 22:5, 6
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 5 Aliwatuma wajumbe kwa Balaamu mwana wa Beori huko Pethori,+ karibu na Mto Efrati katika nchi yake. Alimwambia hivi: “Sasa, kuna watu ambao wametoka Misri. Wamejaa kila mahali duniani,*+ na wanakaa papa hapa karibu nami. 6 Basi, tafadhali, njoo uwalaani watu hawa kwa niaba yangu,+ kwa maana wana nguvu kuliko mimi. Huenda nikawashinda na kuwafukuza kutoka nchini, kwa maana najua vema kwamba yule unayembariki amebarikiwa na yule unayemlaani amelaaniwa.”

  • Hesabu 23:7
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 7 Kisha akasema maneno haya ya kishairi:+

      “Balaki mfalme wa Moabu amenileta kutoka Aramu,+

      Kutoka katika milima ya mashariki:

      ‘Njoo umlaani Yakobo kwa niaba yangu.

      Naam, njoo uwashutumu Waisraeli.’+

  • Hesabu 23:11
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 11 Ndipo Balaki akamwambia Balaamu: “Kwa nini umenitendea hivi? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini badala yake umewabariki tu.”+

  • Hesabu 24:10
    Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
    • 10 Ndipo Balaki akamkasirikia sana Balaamu. Akapiga makofi kwa dharau na kumwambia Balaamu: “Nilikuita uwalaani maadui wangu,+ badala yake umewabariki mara tatu.

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki