-
Zaburi 105:27-36Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
27 Walifanya ishara zake kati yao,
Miujiza yake katika nchi ya Hamu.+
28 Alilituma giza na nchi ikawa giza;+
Hawakuasi maneno yake.
29 Alibadili maji yao yakawa damu
Na kuwaua samaki wao.+
30 Nchi yao ikajaa vyura,+
Hata katika vyumba vya mfalme.
33 Aliipiga mizabibu yao na mitini yao
Na kuivunjavunja miti ya eneo lao.
34 Aliagiza nzige wavamie,
Nzige wachanga wasio na idadi.+
35 Walikula kabisa mimea yote nchini,
Nao wakala kabisa mazao ya ardhi.
36 Kisha akamuua kila mzaliwa wa kwanza katika nchi yao,+
Mwanzo wa nguvu zao za uzazi.
-