-
Kumbukumbu la Torati 28:49-51Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
49 “Yehova ataleta dhidi yenu taifa la mbali,+ kutoka mwisho wa dunia; litawarukia kama tai,+ taifa ambalo hamtaelewa lugha yake,+ 50 taifa lenye uso mkali ambalo haliwajali wazee wala kuwahurumia vijana.+ 51 Watu hao watawala watoto wa mifugo yenu na mazao ya ardhi yenu mpaka mtakapokuwa mmeangamizwa. Hawatawaachia nafaka yoyote, divai mpya wala mafuta, ng’ombe mchanga wala mwanakondoo mpaka watakapokuwa wamewaangamiza.+
-
-
Yeremia 5:17Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
-
-
17 Watakula mavuno yenu na mkate wenu.+
Watawala wana wenu na mabinti wenu.
Watayala makundi yenu na mifugo yenu.
Wataila mizabibu yenu na mitini yenu.
Watayaangamiza kwa upanga majiji yenu yenye ngome mnayoyatumaini.”
-