Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ayubu 18
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

Ayubu—Yaliyomo

      • Bildadi azungumza kwa mara ya pili (1-21)

        • Aeleza yatakayowapata waovu (5-20)

        • Adai Ayubu hamjui Mungu (21)

Ayubu 18:1

Marejeo

  • +Ayu 2:11; 8:1

Ayubu 18:3

Maelezo ya Chini

  • *

    Au labda, “wasio safi.”

Marejeo

  • +Zb 73:22

Ayubu 18:4

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “ukiirarua nafsi yako.”

Ayubu 18:5

Marejeo

  • +Ayu 8:13, 14; 11:20

Ayubu 18:7

Marejeo

  • +Ayu 5:13

Ayubu 18:9

Marejeo

  • +Ayu 5:5; 22:5, 10

Ayubu 18:11

Marejeo

  • +Ayu 15:21; 20:25

Ayubu 18:12

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “achechemee.”

Marejeo

  • +Ayu 15:23

Ayubu 18:13

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Mzaliwa wa kwanza wa kifo anakula.”

Ayubu 18:14

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kifo kinachotisha.”

Marejeo

  • +Ayu 11:20

Ayubu 18:15

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “Kitu ambacho si chake kitakaa.”

Marejeo

  • +Kum 29:22, 23

Ayubu 18:17

Maelezo ya Chini

  • *

    Tnn., “hatakuwa na jina.”

Ayubu 18:18

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “kwenye ardhi inayozaa.”

Ayubu 18:19

Maelezo ya Chini

  • *

    Au “makao yake ya muda.”

Jumla

Ayu. 18:1Ayu 2:11; 8:1
Ayu. 18:3Zb 73:22
Ayu. 18:5Ayu 8:13, 14; 11:20
Ayu. 18:7Ayu 5:13
Ayu. 18:9Ayu 5:5; 22:5, 10
Ayu. 18:11Ayu 15:21; 20:25
Ayu. 18:12Ayu 15:23
Ayu. 18:14Ayu 11:20
Ayu. 18:15Kum 29:22, 23
  • Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
  • 6
  • 7
  • 8
  • 9
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
  • 15
  • 16
  • 17
  • 18
  • 19
  • 20
  • 21
Tafsiri ya Ulimwegu Mpya
Ayubu 18:1-21

Ayubu

18 Bildadi+ Mshua akajibu:

 2 “Utaendelea kusema maneno haya mpaka lini?

Onyesha uelewaji kidogo ili nasi tuseme.

 3 Kwa nini tuonwe kama wanyama+

Na kuonekana wapumbavu* machoni pako?

 4 Hata ukijirarua* vipandevipande kwa hasira,

Je, dunia itaachwa kwa ajili yako,

Au mwamba kuhama mahali pake?

 5 Naam, nuru ya mwovu itazimwa,

Na mwali wa moto wake hautang’aa.+

 6 Hakika nuru iliyo ndani ya hema lake itakuwa giza,

Na taa iliyo juu yake itazimwa.

 7 Hatua zenye nguvu zimefupishwa,

Na shauri lake mwenyewe litamwangusha.+

 8 Kwa maana miguu yake itamwongoza kwenye wavu,

Naye atatangatanga kwenye kamba za wavu.

 9 Mtego utamnasa kisigino;

Na kitanzi kitamkamata.+

10 Kamba imefichwa ardhini kwa ajili yake,

Na mtego uko kwenye kijia chake.

11 Vitisho vinamwogopesha pande zote+

Na kumfuatia miguuni pake.

12 Nguvu zake zimepungua,

Na msiba+ utamfanya ayumbeyumbe.*

13 Ngozi yake imeliwa;

Ugonjwa hatari sana unakula* viungo vyake.

14 Ameng’olewa kutoka katika hema lake lililo salama+

Na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.*

15 Wageni watakaa* katika hema lake;

Kiberiti kitatawanywa juu ya makao yake.+

16 Chini yake, mizizi yake itakauka,

Na juu yake, matawi yake yatanyauka.

17 Hakuna atakayemkumbuka duniani,

Na jina lake halitajulikana* mtaani.

18 Ataondolewa kwenye nuru na kupelekwa gizani

Na kufukuzwa kutoka duniani.*

19 Hatakuwa na mtoto wala mzao miongoni mwa watu wake,

Wala hakuna atakayebaki katika makao yake.*

20 Siku yake itakapofika, watu wa Magharibi watashtuka sana

Na watu wa Mashariki watashikwa na hofu.

21 Hivyo ndivyo inavyokuwa kwa mahema ya mkosaji

Na kwa makao ya mtu ambaye hajamjua Mungu.”

Tanzanian sign language publications(2020-2025)
Toka
Ingia
  • Lugha ya Alama ya Tanzania
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki