Tafsiri ya Ulimwegu Mpya Isaya—Yaliyomo ISAYA YALIYOMO 1 Baba na wanawe waasi (1-9) Yehova anachukia ibada ya kidesturi (10-17) “Tunyooshe mambo kati yetu” (18-20) Sayuni litakuwa jiji lenye uaminifu tena (21-31) 2 Mlima wa Yehova wainuliwa (1-5) Panga zitakuwa majembe ya plau (4) Siku ya Yehova itawafedhehesha wenye majivuno (6-22) 3 Viongozi wa Yuda wawapotosha watu (1-15) Mabinti wa Sayuni wanaotongoza wahukumiwa (16-26) 4 Wanawake saba kwa mwanamume mmoja (1) Atakachochipusha Yehova kitakuwa chenye utukufu (2-6) 5 Wimbo kuhusu shamba la Yehova la mizabibu (1-7) Ole kwa shamba la Yehova la mizabibu (8-24) Hasira ya Mungu dhidi ya watu wake (25-30) 6 Maono ya Yehova katika hekalu lake (1-4) “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Yehova” (3) Midomo ya Isaya yasafishwa (5-7) Isaya atumwa (8-10) “Mimi hapa! Nitume mimi!” (8) “Ni mpaka lini, Ee Yehova?” (11-13) 7 Ujumbe kwa Mfalme Ahazi (1-9) Shear-yashubu (3) Ishara ya Imanueli (10-17) Matokeo ya kutokuwa waaminifu (18-25) 8 Shambulizi linalokuja la Ashuru (1-8) Maher-shalal-hash-bazi (1-4) Usiogope—“Mungu yuko pamoja nasi!” (9-17) Isaya na watoto wake ni kama ishara (18) Tafuteni habari katika sheria, si kwa roho waovu (19-22) 9 Nuru kuu kwa ajili ya nchi ya Galilaya (1-7) “Mkuu wa Amani” azaliwa (6, 7) Mkono wa Mungu dhidi ya Israeli (8-21) 10 Mkono wa Mungu dhidi ya Israeli (1-4) Ashuru—Fimbo ya hasira ya Mungu (5-11) Ashuru kuadhibiwa (12-19) Watu waliobaki wa Yakobo watarudi (20-27) Mungu atahukumu Ashuru (28-34) 11 Utawala wa uadilifu wa tawi la Yese (1-10) Mbwamwitu na mwanakondoo watakaa pamoja (6) Ujuzi kumhusu Yehova utajaa duniani (9) Waliobaki watarudishwa (11-16) 12 Wimbo wa shukrani (1-6) “Yah Yehova ni nguvu zangu” (2) 13 Tangazo dhidi ya Babiloni (1-22) Siku ya Yehova iko karibu! (6) Wamedi kuangusha Babiloni (17) Babiloni halitakaliwa kamwe (20) 14 Waisraeli wataishi katika nchi yao (1, 2) Dhihaka dhidi ya mfalme wa Babiloni (3-23) Anayeng’aa ataanguka kutoka mbinguni (12) Mkono wa Yehova utamponda Mwashuru (24-27) Tangazo dhidi ya Ufilisti (28-32) 15 Tangazo dhidi ya Moabu (1-9) 16 Ujumbe dhidi ya Moabu waendelea (1-14) 17 Tangazo dhidi ya Damasko (1-11) Mataifa yatakemewa na Yehova (12-14) 18 Ujumbe dhidi ya Ethiopia (1-7) 19 Tangazo dhidi ya Misri (1-15) Wamisri watamjua Yehova (16-25) Madhabahu kwa ajili ya Yehova nchini Misri (19) 20 Ishara dhidi ya Misri na Ethiopia (1-6) 21 Tangazo dhidi ya nyika ya bahari (1-10) Kulinda kwenye mnara wa mlinzi (8) “Babiloni ameanguka!” (9) Tangazo dhidi ya Duma na nchi tambarare ya jangwani (11-17) “Mlinzi, kuna habari gani za usiku?” (11) 22 Tangazo kuhusu Bonde la Maono (1-14) Eliakimu awa msimamizi badala ya Shebna (15-25) Kigingi cha mfano (23-25) 23 Tangazo dhidi ya Tiro (1-18) 24 Yehova ataifanya nchi kuwa tupu (1-23) Yehova ni Mfalme katika Sayuni (23) 25 Baraka nyingi kwa watu wa Mungu (1-12) Karamu ya Yehova ya divai bora (6) Kifo hakitakuwepo tena (8) 26 Wimbo kuhusu tumaini na wokovu (1-21) Yah Yehova, Mwamba wa milele (4) Watu duniani watajifunza uadilifu (9) “Wafu wako wataishi” (19) Ingieni katika vyumba vya ndani mjifiche (20) 27 Yehova amuua Lewiathani (1) Wimbo kuhusu Israeli likiwa shamba la mizabibu (2-13) 28 Ole kwa walevi wa Efraimu! (1-6) Makuhani na manabii wa Yuda wapepesuka (7-13) “Agano na Kifo” (14-22) Jiwe la pembeni lenye thamani katika Sayuni (16) Kazi ya Yehova isiyo ya kawaida (21) Mfano kuhusu nidhamu ya Yehova yenye hekima (23-29) 29 Ole kwa Arieli! (1-16) Ibada ya midomo tu yashutumiwa (13) Viziwi watasikia; na vipofu wataona (17-24) 30 Msaada wa Misri ni bure kabisa (1-7) Watu wakataa ujumbe wa kinabii (8-14) Mtakuwa na nguvu mkiendelea kuwa na tumaini (15-17) Yehova awaonyesha kibali watu wake (18-26) Yehova, Mfundishaji Mkuu (20) “Hii ndiyo njia” (21) Yehova atatekeleza hukumu dhidi ya Ashuru (27-33) 31 Msaada wa kweli unatoka kwa Mungu, hautoki kwa wanadamu (1-9) Farasi wa Misri ni nyama tu (3) 32 Mfalme na wakuu watatawala kwa haki ya kweli (1-8) Wanawake wanaopuuza mambo waonywa (9-14) Kumiminwa kwa roho kwaleta baraka (15-20) 33 Hukumu na tumaini kwa waadilifu (1-24) Yehova ni Mwamuzi, Mpaji-sheria, na Mfalme (22) Hakuna atakayesema: “Mimi ni mgonjwa” (24) 34 Kisasi cha Yehova dhidi ya mataifa (1-8) Edomu itafanywa ukiwa (9-17) 35 Paradiso yarudishwa (1-7) Vipofu wataona; viziwi watasikia (5) Njia ya Utakatifu kwa ajili ya waliokombolewa (8-10) 36 Senakeribu ashambulia Yuda (1-3) Rabshake amdhihaki Yehova (4-22) 37 Hezekia atafuta msaada wa Mungu kupitia Isaya (1-7) Senakeribu atishia Yerusalemu (8-13) Sala ya Hezekia (14-20) Isaya apeleka jibu la Mungu (21-35) Malaika awaua Waashuru 185,000 (36-38) 38 Hezekia ashikwa na ugonjwa kisha apona (1-22) Wimbo wa shukrani (10-20) 39 Wajumbe kutoka Babiloni (1-8) 40 Faraja kwa watu wa Mungu (1-11) Sauti nyikani (3-5) Ukuu wa Mungu (12-31) Mataifa kama tone kutoka katika ndoo (15) Mungu hukaa “juu ya duara ya dunia” (22) Nyota zote huitwa kwa majina (26) Mungu hachoki kamwe (28) Wanaomtumaini Yehova watapata nguvu mpya (29-31) 41 Mshindi kutoka mashariki (1-7) Israeli achaguliwa kuwa mtumishi wa Mungu (8-20) “Rafiki yangu Abrahamu” (8) Miungu mingine yajaribiwa (21-29) 42 Mtumishi wa Mungu na kazi yake (1-9) ‘Jina langu ni Yehova’ (8) Wimbo mpya wa kumsifu Yehova (10-17) Israeli ni kipofu na kiziwi (18-25) 43 Yehova awakusanya tena watu wake (1-7) Miungu yashtakiwa (8-13) “Ninyi ni mashahidi wangu” (10, 12)(10, 12) Waachiliwa huru kutoka Babiloni (14-21) “Tukutane ili tufanye kesi” (22-28) 44 Baraka kwa watu waliochaguliwa na Mungu (1-5) Hakuna Mungu ila Yehova (6-8) Upumbavu wa sanamu zilizotengenezwa na wanadamu (9-20) Yehova, Mkombozi wa Israeli (21-23) Ukombozi kupitia Koreshi (24-28) 45 Koreshi atiwa mafuta ili aliteke Babiloni (1-8) Udongo haupaswi kushindana na Mfinyanzi (9-13) Mataifa mengine yatambua Israeli (14-17) Mungu anategemeka katika uumbaji na katika kufunua mambo (18-25) Dunia iliumbwa ili ikaliwe (18) 46 Sanamu za Babiloni dhidi ya Mungu wa Israeli (1-13) Yehova atabiri mambo ya wakati ujao (10) Ndege anayewinda anayetoka mashariki (11) 47 Kuanguka kwa Babiloni (1-15) Wanajimu wafunuliwa (13-15) 48 Watu wa Israeli wakemewa na kusafishwa (1-11) Yehova atachukua hatua dhidi ya Babiloni (12-16a) Mafundisho ya Mungu ni yenye faida (16b-19) “Tokeni Babiloni!” (20-22) 49 Kazi ya mtumishi wa Yehova (1-12) Nuru ya mataifa (6) Faraja kwa Waisraeli (13-26) 50 Dhambi za Waisraeli zasababisha matatizo (1-3) Mtumishi mtiifu wa Yehova (4-11) Ulimi na sikio la waliofundishwa (4) 51 Sayuni larudishwa kuwa kama bustani ya Edeni (1-8) Faraja kutoka kwa Muumba wa Sayuni mwenye nguvu (9-16) Kikombe cha ghadhabu ya Yehova (17-23) 52 Amka, Ee Sayuni! (1-12) Miguu ya wale wanaoleta habari njema inapendeza (7) Walinzi wa Sayuni wapaza sauti kwa pamoja (8) Wale wanaobeba vyombo vya Yehova lazima wawe safi (11) Mtumishi wa Yehova atakwezwa (13-15) Sura iliyoharibika (14) 53 Kuteseka, kufa, na kuzikwa kwa mtumishi wa Yehova (1-12) Adharauliwa na kuepukwa (3) Abeba magonjwa na maumivu (4) “Kama kondoo machinjioni” (7) Abeba dhambi za wengi (12) 54 Sayuni aliye tasa atapata wana wengi (1-17) Yehova ni mume wa Sayuni (5) Wana wa Sayuni watafundishwa na Yehova (13) Silaha dhidi ya Sayuni zitashindwa (17) 55 Mwaliko wa kula na kunywa bure (1-5) Mtafuteni Yehova na neno lake linalotegemeka (6-13) Njia za Mungu ziko juu kuliko njia za mwanadamu (8, 9) Neno la Mungu hakika litafanikiwa (10, 11) 56 Baraka kwa wageni na matowashi (1-8) Nyumba ya sala kwa ajili ya wote (7) Walinzi vipofu, mbwa walio bubu (9-12) 57 Mtu mwadilifu na watu washikamanifu waangamia (1, 2) Ukahaba wa kiroho wa Israeli wafunuliwa (3-13) Faraja kwa watu wa hali ya chini (14-21) Waovu ni kama bahari iliyochafuka (20) Hakuna amani kwa waovu (21) 58 Kufunga kwa kweli na kwa uwongo (1-12) Kushika Sabato kwa furaha (13, 14) 59 Dhambi za Waisraeli zawatenga na Mungu (1-8) Kuungama dhambi (9-15a) Yehova huingilia kati kwa ajili ya wanaotubu (15b-21) 60 Utukufu wa Mungu wang’aa juu ya Sayuni (1-22) Kama njiwa kwenye viota vyao (8) Dhahabu badala ya shaba (17) Mdogo atakuwa elfu (22) 61 Atiwa mafuta ili kutangaza habari njema (1-11) “Mwaka wa nia njema ya Yehova” (2) “Miti mikubwa ya uadilifu” (3) Watu wa nchi nyingine watasaidia (5) “Makuhani wa Yehova” (6) 62 Jina jipya la Sayuni (1-12) 63 Kisasi cha Yehova dhidi ya mataifa (1-6) Upendo mshikamanifu wa Yehova nyakati za zamani (7-14) Sala ya toba (15-19) 64 Sala ya toba yaendelea (1-12) Yehova “Mfinyanzi wetu” (8) 65 Hukumu ya Yehova dhidi ya wanaoabudu sanamu (1-16) Mungu wa Bahati Njema na Mungu wa Majaliwa (11) “Watumishi wangu watakula” (13) Mbingu mpya na dunia mpya (17-25) Kujenga nyumba; kupanda mashamba ya mizabibu (21) Hakuna atakayefanya kazi ngumu bure (23) 66 Ibada ya kweli na ibada ya uwongo (1-6) Sayuni na wanawe (7-17) Watu wakusanyika Yerusalemu ili kuabudu (18-24)