Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Lugha ya Alama ya Tanzania
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lmd 5
  • Busara

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Busara
  • Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Paulo Alifanya Nini
  • Tunajifunza Nini Kutoka kwa Paulo?
  • Mwige Paulo
  • Unyenyekevu
    Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Kupendezwa na Watu
    Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Kuzungumza kwa Njia ya Kawaida
    Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
  • Fadhili
    Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
Pata Habari Zaidi
Wapende Watu—Fanya Wanafunzi
lmd 5

KUANZISHA MAZUNGUMZO

Mtume Paulo akijadiliana na watu wa Athene.

Matendo 17:​22, 23

SOMO LA 5

Busara

Kanuni: “Maneno yenu na yawe yenye neema sikuzote.”—Kol. 4:6.

Paulo Alifanya Nini

Mtume Paulo akijadiliana na watu wa Athene.

VIDEO: Paulo Anawahubiria Waathene

1. Tazama VIDEO, au soma Matendo 17:​22, 23. Kisha fikiria maswali yafuatayo:

  1. Paulo alihisije kuhusu mazoea ya dini za uwongo aliyoona katika jiji la Athene?—Ona Matendo 17:16.

  2. Badala ya kuwahukumu Waathene, Paulo alitumiaje kwa busara mambo waliyoamini kama njia ya kuwahubiria habari njema?

Tunajifunza Nini Kutoka kwa Paulo?

2. Huenda watu wakatusikiliza zaidi ikiwa tutachagua kwa uangalifu mambo tutakayozungumza, jinsi tutakavyozungumza na wakati wa kuzungumza.

Mwige Paulo

3. Chagua maneno yanayofaa. Kwa mfano, unapozungumza na mtu ambaye si Mkristo, huenda ukahitaji kubadili jinsi unavyoitaja Biblia au unavyomrejelea Yesu.

4. Usiwe na haraka ya kumkosoa mtu. Mruhusu ajieleze. Ikiwa atasema jambo lolote lisilopatana na mafundisho ya Biblia, usibishane naye. (Yak. 1:19) Ukimsikiliza, utajua mambo anayoamini na kwa nini anayaamini.—Met. 20:5.

5. Kubaliana naye na mpongeze inapofaa kufanya hivyo. Huenda anaamini kwamba mafundisho ya dini yake ni sahihi. Kwanza, jaribu kuzungumzia mambo mnayokubaliana, kisha msaidie hatua kwa hatua aelewe mambo ambayo Biblia inafundisha.

SOMA PIA

Met. 25:15; 2 Tim. 2:​23-26; 1 Pet. 3:15

    Tanzanian sign language publications(2020-2025)
    Toka
    Ingia
    • Lugha ya Alama ya Tanzania
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki