23 Ndipo Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwana wake na wanaume wote waliozaliwa nyumbani mwake na kila mtu aliyenunuliwa kwa pesa zake, kila mtu wa kiume kati ya wanaume wa nyumba ya Abrahamu, naye akaanza kutahiri nyama ya magovi yao siku hiyo hiyo, kama Mungu alivyokuwa amemwambia.+