Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Juma Hili
Julai 14-20
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2025 | Julai

JULAI 14-20

METHALI 22

Wimbo 79 na Sala | Utangulizi (Dak. 1)

HAZINA ZA NENO LA MUNGU

1. Kanuni Zenye Hekima za Kuwalea Watoto

(Dak. 10)

Watayarishe watoto wako ili waweze kukabiliana na changamoto maishani (Met 22:3; w20.10 27 ¶7)

Anza kuwazoeza tangu wakiwa wachanga (Met 22:6; w19.12 26 ¶17-19)

Watie nidhamu kwa njia ya upendo (Met 22:15; w06 4/1 9 ¶4)

Kwa fadhili, baba anatumia Biblia kusababu na binti yake. Tablet yake ina picha zinazoonyesha hatua za kinadharia za mageuzi ya binadamu.

2. Hazina za Kiroho

(Dak. 10)

  • Met 22:29—Tunaweza kutumiaje methali hii katika utendaji wetu wa kutaniko, na tutapata manufaa gani? (w21.08 22 ¶11)

  • Ungependa kushiriki nasi hazina gani kutoka kwenye usomaji wa Biblia wa juma hili?

3. Usomaji wa Biblia

(Dak. 4) Met 22:​1-19 (th somo la 10)

BORESHA HUDUMA YAKO

4. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 3) NYUMBA KWA NYUMBA. (lmd somo la 5 jambo kuu la 4)

5. Kuanzisha Mazungumzo

(Dak. 4) MAHUBIRI YASIYO RASMI. Mwonyeshe mtu huyo jinsi ya kupata habari kwenye jw.org inayotoa msaada kwa wazazi. (lmd somo la 1 jambo kuu la 4)

6. Hotuba

(Dak. 5) ijwyp makala ya 100—Kichwa: Vipi Ikiwa Nimevunja Sheria Fulani ya Nyumbani? (th somo la 20)

MAISHA YA MKRISTO

Wimbo 134

7. Uwe na Subira, lakini Usiwaendekeze

(Dak. 15) Mazungumzo.

Kuwalea watoto kunahitaji subira nyingi. Wazazi wanapaswa kuwakazia uangalifu watoto wao kwa ukawaida na kutumia muda wa kutosha pamoja nao. (Kum 6:​6, 7) Ili wazazi wajue yaliyo moyoni mwa watoto wao, wanahitaji kuwauliza maswali, na kusikiliza kwa makini yale ambayo watoto wao wanasema. (Met 20:5) Pia, huenda wazazi wakahitaji kurudia mara nyingi maagizo wanayowapa watoto ili wayaelewe na kuyatumia.

Hata hivyo, wazazi wenye subira, hawawaendekezi watoto wao. Yehova amewapa mamlaka ya kuwawekea watoto wao mipaka na kuwapa nidhamu inayofaa wanapokosa kutii.—Met 6:20; 23:13.

Soma Waefeso 4:31. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Kwa nini wazazi wanapokuwa na hasira, hawapaswi kuwatia nidhamu watoto wao?

Soma Wagalatia 6:7. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Kwa nini wazazi wanapaswa kuwafundisha watoto wao kwamba ikiwa watafanya mambo mabaya watapatwa na matokeo mabaya?

Picha kutoka kwenye video “ ‘Kwa Subira, Vumilianeni kwa Upendo’​—⁠Watoto Wako.” Max anamsikiliza Sue, binti yake, kwa subira.

Onyesha VIDEO YENYE KICHWA ‘Kwa Subira, Vumilianeni kwa Upendo’—Watoto Wako. Kisha waulize wasikilizaji:

  • Umejifunza masomo gani kutokana na video hiyo?

8. Funzo la Biblia la Kutaniko

(Dak. 30)lfb “Barua Kutoka kwa Baraza Linaloongoza,” utangulizi wa sehemu ya 1, na somo la 1

Umalizio (Dak 3.) | Wimbo 6 na Sala

Yaliyomo
Mnara wa Mlinzi (Funzo)—2025 | Mei

Makala ya 19: Julai 14-20, 2025

2 Waige Malaika Waaminifu

Habari za Ziada

Makala nyingine katika gazeti hili

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki