22 Na kipimo cha madirisha yake na ukumbi wake na maumbo yake ya mitende+ kilikuwa sawa na kipimo cha lango ambalo upande wake wa mbele unaelekea mashariki. Na kwa kutumia vipandio saba watu wangeweza kupanda kuingia ndani yake, na ukumbi wake ulikuwa mbele yake.