20 Sasa siku ya tatu ilikuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa Farao,+ kwa hiyo aliwafanyia karamu watumishi wake wote, akamtoa gerezani msimamizi mkuu wa vinywaji na mwokaji mkuu, akawaleta mbele ya watumishi wake. 21 Akamrudisha msimamizi mkuu wa vinywaji kwenye cheo chake, akaendelea kumpa Farao kikombe.