-
Mwanzo 41:48, 49Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
48 Naye aliendelea kukusanya chakula chote cha miaka saba katika nchi ya Misri, akakiweka katika maghala majijini. Katika kila jiji alikusanya chakula kutoka katika mashamba yaliyozunguka jiji hilo. 49 Yosefu akaendelea kukusanya nafaka nyingi sana katika maghala, kama mchanga wa bahari, hivi kwamba mwishowe wakaacha kuipima kwa sababu haingeweza kupimwa.
-