17 Kwa hiyo shamba la Efroni lililokuwa Makpela, mbele ya Mamre—shamba na pango lililokuwemo na miti yote iliyokuwa ndani ya mipaka ya shamba hilo—likathibitishwa kuwa 18 mali ya Abrahamu aliyoinunua mbele ya wana wa Hethi, mbele ya wote walioingia katika lango la jiji lake.