-
Mwanzo 6:19, 20Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Nawe uingize ndani ya safina viumbe hai+ wawili wawili wa kila aina ili kuwahifadhi hai pamoja nawe, dume na jike;+ 20 viumbe wanaoruka angani kulingana na aina zao, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zao, na wanyama wote wanaotambaa kulingana na aina zao, watakuja ndani kwako viumbe wawili wawili wa kila aina ili uwahifadhi hai.+
-
-
Mwanzo 7:14, 15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 Waliingia ndani pamoja na kila mnyama wa mwituni kulingana na aina yake, na kila mnyama wa kufugwa kulingana na aina yake, na kila mnyama anayetambaa duniani kulingana na aina yake, na kila kiumbe anayeruka kulingana na aina yake, kila ndege, kila kiumbe mwenye mabawa. 15 Waliendelea kumjia Noa ndani ya safina, wawili wawili, kila aina ya kiumbe mwenye pumzi ya uhai.*
-