12 Na Mungu akaendelea kusema: “Hii ndiyo ishara ya agano ninalofanya pamoja nanyi na pamoja na kila kiumbe hai aliye pamoja nanyi, kwa vizazi vyote vijavyo. 13 Ninauweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano nililofanya na dunia.