3 naye akamwambia: ‘Ondoka katika nchi yako na kutoka kwa watu wako wa ukoo uje katika nchi nitakayokuonyesha.’+ 4 Ndipo akaondoka katika nchi ya Wakaldayo, akaanza kuishi Harani. Na kutoka hapo, baada ya baba yake kufa,+ Mungu akamwagiza ahamie nchi hii ambayo mnaishi sasa.+