26 Sasa kulikuwa na njaa kali nchini, mbali na ile njaa kali ya kwanza iliyotokea siku za Abrahamu,+ kwa hiyo Isaka akaenda Gerari kwa Abimeleki mfalme wa Wafilisti. 2 Kisha Yehova akamtokea Isaka na kumwambia: “Usishuke kwenda Misri. Kaa katika nchi nitakayokuonyesha.