30 Sasa Isaka alipomaliza tu kumbariki Yakobo na Yakobo alipotoka tu mbele ya Isaka baba yake, Esau ndugu yake akarudi kutoka mawindoni.+ 31 Yeye pia akapika chakula kitamu na kumletea baba yake, akamwambia baba yake: “Baba, amka ule nyama niliyokuletea, ili unibariki.”