-
Kumbukumbu la Torati 17:14, 15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
14 “Mtakapoingia katika nchi ambayo Yehova Mungu wenu anawapa, mkaimiliki na kuishi humo, nanyi mseme, ‘Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yote yanayotuzunguka,’+ 15 mnapaswa kumweka mfalme ambaye Yehova Mungu wenu atamchagua.+ Mnapaswa kumchagua mfalme kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Hamruhusiwi kumweka mfalme ambaye ni mgeni, ambaye si ndugu yenu.
-
-
1 Mambo ya Nyakati 1:43-50Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
43 Hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu+ kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli:*+ Bela mwana wa Beori; jiji lake liliitwa Dinhaba. 44 Bela alipokufa, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra+ alianza kutawala baada yake. 45 Yobabu alipokufa, Hushamu kutoka katika nchi ya Watemani alianza kutawala baada yake. 46 Hushamu alipokufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyewashinda Wamidiani katika eneo* la Moabu, alianza kutawala baada yake. Jiji lake liliitwa Avithi. 47 Hadadi alipokufa, Samla kutoka Masreka alianza kutawala baada yake. 48 Samla alipokufa, Shauli kutoka Rehobothi karibu na ule Mto alianza kutawala baada yake. 49 Shauli alipokufa, Baal-hanani mwana wa Akbori alianza kutawala baada yake. 50 Baal-hanani alipokufa, Hadadi alianza kutawala baada yake. Jiji lake liliitwa Pau, na mke wake aliitwa Mehetabeli binti ya Matredi, binti ya Mezahabu.
-