7 “Msiwape tena watu hawa nyasi za kufyatua matofali.+ Waacheni wakajitafutie nyasi wenyewe. 8 Lakini bado mnapaswa kuwaamuru wafyatue idadi ileile ya matofali kama awali. Msiwapunguzie idadi, kwa sababu wanastarehe. Ndiyo sababu wanalia, ‘Tunataka kwenda, tunataka kumtolea dhabihu Mungu wetu!’