3 Kwa miaka sita mtapanda mbegu katika mashamba yenu, mtapunguza matawi ya mizabibu yenu, na kuvuna mazao ya nchi.+ 4 Lakini katika mwaka wa saba nchi itakuwa na pumziko kamili la sabato, sabato ya Yehova. Hampaswi kupanda mbegu wala kupunguza matawi ya mizabibu yenu.