-
Kutoka 39:19-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Halafu wakatengeneza pete mbili za dhahabu na kuziweka kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani, upande wa efodi.+ 20 Kisha wakatengeneza pete nyingine mbili za dhahabu upande wa mbele wa efodi, chini ya vipande viwili vya mabegani vya efodi, karibu na mahali inapoungana, juu ya mshipi uliofumwa wa efodi. 21 Hatimaye, wakafunga pete za kifuko cha kifuani pamoja na pete za efodi kwa kamba ya bluu, ili kifuko cha kifuani kibaki mahali pake kwenye efodi, juu ya mshipi uliofumwa, kama Yehova alivyomwamuru Musa.
-