-
Kutoka 29:24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Ni lazima uviweke vitu hivyo vyote mikononi mwa Haruni na mikononi mwa wanawe, nawe utavitikisa kwenda mbele na nyuma vikiwa toleo la kutikiswa mbele za Yehova.
-
-
Mambo ya Walawi 8:25-27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Kisha akachukua yale mafuta, mkia wenye mafuta, mafuta yote yaliyofunika matumbo, mafuta yote yaliyokuwa juu ya ini, zile figo mbili na mafuta yake, na mguu wa kulia.+ 26 Akachukua mkate mmoja wa mviringo usio na chachu,+ mkate mmoja wa mviringo wenye mafuta,+ na mkate mmoja mwembamba kutoka katika kikapu cha mikate isiyo na chachu kilichokuwa mbele za Yehova. Akaiweka mikate hiyo juu ya vipande vya mafuta na juu ya mguu wa kulia. 27 Baada ya hayo akaviweka vitu hivyo vyote katika mikono ya Haruni na mikono ya wanawe na kuanza kuvitikisa kwenda mbele na nyuma vikiwa toleo la kutikiswa mbele za Yehova.
-