-
Mambo ya Walawi 8:15, 16Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Musa akamchinja, akachukua damu yake+ kwa kidole chake na kuzipaka pembe zote za madhabahu, akaitakasa madhabahu kutokana na dhambi, lakini damu iliyobaki aliimwaga kwenye msingi wa madhabahu, ili aitakase na kutoa juu yake dhabihu ya kufunika dhambi. 16 Kisha Musa akachukua mafuta yote yaliyofunika matumbo, mafuta yaliyo juu ya ini, na figo mbili pamoja na mafuta yake, akateketeza vitu hivyo juu ya madhabahu ili vifuke moshi.+
-