6 Au mtatoa kondoo dume pamoja na sehemu mbili za kumi za kipimo cha efa moja ya unga laini uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kwa ajili ya toleo la nafaka. 7 Nanyi mnapaswa kutoa sehemu ya tatu ya hini ya divai ili iwe toleo la kinywaji lenye harufu inayompendeza Yehova.