15 Nchi ambayo watu wa kabila la Yuda waligawiwa+ kwa ajili ya koo zao ilifika kwenye mpaka wa Edomu,+ nyika ya Zini, hadi upande wa kusini kabisa wa Negebu. 2 Mpaka wao wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,+ yaani, kuanzia mahali ambapo mto unaingia baharini upande wa kusini.