-
Kutoka 29:23, 24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
23 Chukua pia mkate wa mviringo na mkate wa mviringo uliokandwa kwa mafuta na mkate mwembamba kutoka katika kile kikapu cha mikate isiyo na chachu kilicho mbele za Yehova. 24 Ni lazima uviweke vitu hivyo vyote mikononi mwa Haruni na mikononi mwa wanawe, nawe utavitikisa kwenda mbele na nyuma vikiwa toleo la kutikiswa mbele za Yehova.
-