15 Kwa siku saba mtakula mikate isiyo na chachu.+ Naam, siku ya kwanza mtaondoa nyumbani mwenu unga uliokandwa wenye chachu, kwa sababu mtu yeyote atakayekula kitu kilichotiwa chachu kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, ni lazima auawe kutoka katika Israeli.