8 Musa akaendelea kusema: “Yehova atakapowapa nyama ya kula jioni na mikate mtakayokula asubuhi na kushiba, mtajua kwamba Yehova amesikia manung’uniko yenu mnayonung’unika dhidi yake. Lakini sisi ni nani? Hamnung’uniki dhidi yetu, bali dhidi ya Yehova.”+